Wito umetolewa kwa wazazi katika wadi ya Cheptais eneo bunge la Mlima Elgon kuwa waangalifu kwa kuwapa wanao malezi bora wakati watapokuwa nyumbani kwa likizo fupi ili kuwaepusha kupotoka kimaadili.

Ni wito ambao umetolewa na mwenyekiti wa maendeleo ya akina mama wadi ya Cheptais Ann Bucheche ambaye amewasihi wazazi kuwahusisha wanao kwenye shughuli za nyumbani, kando na kuwapa mwelekeo ulio bora utakaowaepusha kujiingiza kwenye visa vya maadili potovu watakapokuwa nyumbani kwa likizo fupi.

Wakati uo huo bi Bucheche amesikitikia idadi kubwa ya visa vya mimba miongoni mwa wanafunzi kaunti hii ya Bungoma na kuwataka wazazi kutilia maanani elimu ya wanao ili kuwawezesha kujikimu siku za usoni.

Bi Bucheche ambaye pia ni mwanaharakati wa amani amezitaka jamii za eneobunge la Mlima Elgon kuzidi kuishi kwa amani na kutumia njia mwafaka kutatua mizozo ya kifamilia.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE