Lushea ndiyo mabingwa wa kombe la CDF eneobunge la Mumias Mashariki baada ya kuwatimba Eluche mabao 2-1 kwenye chuo cha matibabu Cha Shianda KMTC hapo Jana
Mshambulizi pilipili John Khanda alifungua ukurasa wa mabao upande wa Lushea alipotinga bao la kwanza dakika 11 za kipindi Cha kwanza kabla ya Sumba Baya kurejea na kuisawazishia Eluche hivyo kufanya kipindi Cha kwanza kuishia kwa sare ya 1-1
Hatimaye kizaazaa kwenye lango la Eluche kilisababisha bao la pili na kuwafanya Lushea kuibuka washindi wa kombe hilo mwaka 2021
Washindi walitia kibindoni takriban shilingi 30,000 Eluche wakaponyoka na kitita cha shilingi 20,000 Isongo walomaliza wa 3 wakaridhika na shilingi 15,000 huku nambari nne ambao ni Shianda wakitoweka na bunda la shilingi 10,000 pesa taslim
Shianda Accademy walituzwa Kama timu bora ya vijana chini ya umri wa miaka 13, Ekero wakatwaa ubingwa wa Voliboli, Lubinu wakaibuka kidedea Netiboli kinadada huku Ebusia wakitawazwa mabingwa Kandanda kinadada vilevile
Washindi wote kuanzia nambari 1 Hadi 4 walipewa vikombe, mipira pamoja na sare
Mfadhili wa kombe hilo ambaye pia ndiye mbunge wa Mumias Mashariki Ben Washiali amesema kuwa wanalenga kuimarisha soka haswa ya kinadada
Hata hivyo amewatahadharisha wanasiasa dhidi ya kuingiza siasa kwenye swala hilo
Story by James Nandwa