Kiranja wa zamani kwenye bunge la kitaifa Ben Washiali amewarai wakaazi wa jamii ya mulembe kuhakikisha kuwa wanasalia serikalini ili kunufaika pakubwa na maendeleo haswa mashinani
Akizungumza sokoni Shianda eneobunge la Mumias Mashariki Washiali ametaja ujenzi wa chuo cha matibabu Cha Shianda KMTC kama mojawapo ya matunda ya kufanya kazi na serikali
Washiali amechukua fursa hiyo kumpigia debe chama Cha UDA kilichozinduliwa hivi maajuzi akisema kuwa ndicho Chama pekee kitakachojali maslahi ya walala hoi
Mbunge huyo wa Mumias Mashariki amemtaka Kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi kufanya kazi na naibu rais iwapo ananuiya kuwa katika serikali ya baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2022
STORY BY JAMES NANDWA