Shule ya upili ya marafiki ya Kimabole katika eneobunge la Mlima Elgon ni ya hivi punde kukumbwa na visa vya moto baada ya maabara ya shule hiyo kuteketea usiku wa kuamkia leo.

Moto huo ambao chanzo chake hakijabainika ulianza mwendo wa saa tisa asubuhi ya leo umeathiri pakubwa shughuli za shule hiyo ambapo afisi za idara mbalimbali ikiwemo ile ya mitihani, ya mwelekezi wa masomo, ya sayanzi miongoni mwa idara zingine zimeathirika.

Inaarifiwa kuwa wanakijiji walijaribu kuuzima moto huo japo juhudi zao zikafeli.

Kisa hiki ni miongoni mwa visa mbalimbali ambavyo vimeripotiwa kaunti hii ya Bungoma baada ya shule ya Namwela, Kimilili, Chesamisi miongoni mwa shule zingine kuathirika.

Story by Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE