Wakaazi wa eneo bunge la Malava kaunti ya Kakamega wametakiwa kuendelea kufata masharti yaliyotolewa na wizara ya afya ya kupigana na janga la korona la sivyo maisha yao imo hatarini.
Akizungumza na idhaa hii afisini mwake afisa mkuu wa afya eneo hilo Fred Amudavi, ameonya kuwa kuna uwezekano wa virusi hivyo kusambaa Zaidi mwingoni mwa wakaazi hao endapo hatua za kiafya hazitazingatiwa kikamilifu.
“Corona bado iko tafadhali watu wa Malava twendeleee kuvalia barakoa kwa maana ukikupata hauna tiba na utakufa.”
Aidha amudavi ametumia fursa hiyo kuwashauri wazazi kuhakikisha watoto walio chini kati ya miaka miwili na kumi nan ne wanapokea chanjo ya kuzuiya minyoo kwenye zoezi litakalo ng’oa nanga hapo kesho
Story by Imelda Lihavi