Manchester city walijikatia tiketi ya kuingia fainali ya kombe la EUFA baada ya kushinda hapo Jana dhidi ya PSG mabao 2-0 wakiwa na jumla ya mabao 3-1 Huku Leo ikiwa ni zamu ya Chelsea na Real Madrid kuonyesha ubigwa wao

Hayo yakijiri Manchester United imejiunga na mahasimu wa ligi ya primia Tottenham na West Ham katika kinyang’anyiro cha msajili mlinda mlango wa West Brom Sam Johnstone mwenye umri wa miaka 28 ikijiandaa kuondoka kwa Mhispania David de Gea mwenye umri wa miaka 30, msimu huu wa joto.

Kando na hayoMlinzi wa zamani wa England Sol Campbell ni miongoni mwa wale walioomba nafasi ya kuwa mbadala wa Aidy Boothroyd katika nafasi ya meneja wa kikosi cha England kwa wachezaji wa chini ya miaka 21.

By Samson Nyongesa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE