Wabunge wa chama cha ANC kaunti ya Kakamega wameenddelea kupigia debe azma ya kinara wa chama chao Musalia Mudadi kutwaa wadhifa wa urais kwenye kinyang’anyiro cha urais mmwaka wa 2022.

Mbunge wa matungu peter oscar nabulindo anasema mudavadi amekomaa kisiasa na ana tajriba ya kutosha kuongoza taifa hili baada ya muhula wa rais Uhuru Kenyatta kutamatika.

Kauli ambayo imeungwa mkono na katibu wa vuguvugu la youths for Musalia kanda ya Magharibi Brian  Amakobe ambaye anawataka viongozi wa kisiasa kutoka Magharibi kumuunga mkono Mudavadi.

Akizungumza katika eneo la Indangalasia Nabulindo aidha amewataka wakaazi wa Magharibi  kujiandikiza kama wapiga kura ili kuwa na uwezo wa kuamua mstakabali wa siasa za taifa hili.  

By James Nadwa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE