Hali ya huzuni imetanda katika kijiji cha Lusumu wadi ya Kabras West eneo bunge la Malava hii ni baada ya watu wawili wa familia moja kuawa usiku wa kuamkia leo kufuatia mzozo wa kinyumbani 

Kwenye kisa cha kwanza inadaiwa Joseph Onyango mwenye umri wa miaka 39 ambaye ni baba wa watoto kumi aliuawa kwa kukatwakatwa kwa jembe na nduguye mdogo kwa jina Benson Oponyo baada ya wawili hao kutoafautiana kuhusu uchungaji wa mifugo wa boma hilo kabla ya wenyeji waliyokuwa na ghadhabu kumshambulia mzee wa boma hilo wa miaka 76 kwa jina Alfred Ambululi na kumuua papo hapo kama ishara ya kulipiza kisasi .

Ni kisa kilichowaacha wengi wa jamaa, ndugu na marafiki wa wendazao ambao wamehoji kuwa mzozo huo umekuwa ukiendelea kwa muda mrefu kabla ya maafa hayo kutokea.

Hata hivyo miili ya wawili hao itazikiwa kulingana na mila nadesturi ya ukoo wa Abarefi huku tambiko la  aina mbalimbali likitarajiwa kuendeshwa.

Chifu wa kata ya Lukume Maliki Shanguya amethibitisha kisa hicho huku akiwaonya wananchi dhidi ya kujichukulia sheria mikononi mwao.

By Lihavi Imelda

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE