Shinikizo zinazidi kutolewa kwa kinara wa chama cha ODM Raila Odinga kuunga mkono azma ya gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya kupeperusha bendera ya chama cha ODM kwenye kinyang’anyiro cha urais mwaka wa 2022

Aliyekua waziri wa michezo Rashid Echesa anasema kwa muda mrefu eneo la Magharibi limemuunga mkono Raila Ondinga na sasa ni wakati mwafaka kwa odinga kutoa nafasi kwa Oparanya kupeperusha bendera ya chama hicho

Usemi wake unajiri saa chache tu baada ya usemi sawia kutolewa na gavana Wycliffe Oparanya ambaye alisisitiza kuwa amekomaa kisiasa na ana tajriba ya kutosha kuongza taifa hili baada ya muhula wa rais Uhuru Kenyatta kutamatika.

Akizungumza katika eneo la Shibale eneo bunge la  Mumias Magharibi Echesa aidha amewataka wakenya kuzingatia masharti ya wizara ya afya ili kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona

By James Nadwa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE