Serikali ya kaunti ya Kakamega imempokonya mkulima mmoja ng”ombe wa maziwa aliyopewa na serikali ya kaunti hiyo kutoka kijiji cha Mukhamala wadi ya Mahiakalo eneo bunge la Lurambi baada ya mkulima huyo kuuza ndama aliyezaliwa na ng”ombe huyo wa miezi 6.
Akizungumza na kituo hiki wakati wa kumchukuwa ng”ombe huyo kutoka kwa Elfhas Liloko , mtawala wa kaunti hiyo anayesimamia wadi hiyo ya Mahiakalo David Lutta amekashfu kitendo hicho akisema kuwa mkulima huyo aliuza ndama huyo kwa mkulima mwingine ambaye naye alimuuza ndama huyo wa kike kwenye soko la Lubao huku akisema kuwa mshukiwa pia alikuwa akipanga kumuuza ng”ombe huyo.
Hata hivyo mtawala huyo aliamua kumpokonya mkulima huyo ng’ombe huyo na kumkabidhi jirani wake Erick Achevi huku akitumia fursa hiyo kuwaonya walio na tamaa ya kuwauza mifugo waliopewa na serikali kuwaondoa kwenye lindi la umaskini kuwa chuma chao ki motoni na kumpa Elphas siku saba kumrejesha ndama mwingine.
By Linda Adhiambo