Baadhi ya wakaazi wa kijiji cha Ileho eneo bunge la Shinyalu kaunti ya Kakamega wanataka serikali kuwasaidia kurejeshewa mashamba yao ambayo wanadai yalinyakuliwa na kujumuishwa kwa ardhi ya msitu wa Kakamega.

Haya yanajiri siku chache tu baada ya serikali kupitia kwa wizara ya ardhi kuzindua mfumo mpya wa dijitali wa huduma za ardhi

Wazee wa kijiji hicho wakiongozwa na John Matasio wanasema waliwasilisha kesi hiyo ya kunyakuliwa kwa mashamba yao mahakamani mwaka wa 1992, lakini hadi kufikia sasa hawajapata haki

Wanasema wanahofia watapoteza mashamba hayo baada ya kuzinduliwa kwa mfumo mpya wa usimamizi wa ardhi huku wakiitaka serikali kuwasaidia

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE