Vuguvugu la Youths for Mulasia linalounga azma ya Kiongozi wa ANC ya kuwania urais mwakani sasa linamshinikiza naiburais kujiuzulu iwapo haridhiki na uongozi wa serkali iliyopo
Katibu wa vuguvugu hilo Kanda ya Magharibi Brian Amakobe amemtaka Ruto kuondoka serikalini badala ya kuilaumu kila uchao
Amakobe amesema kuwa serikali ya jubilee imefeli kuwahudumia Wakenya na Ruto ni sehemu ya uongozi huo
Kiongozi huyo amemsuta mbunge wa Mumias Mashariki Ben Washiali kwa kuchangia kudorora kwa uchumi eneo hilo
Kiongozi huyo amechukua fursa hiyo kumpigia debe Kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi akisisitiza kuwa ndiye aliye na uwezo wa kuufufua uchumi wa taifa hili unaozidi kudorora
By Richard Milimu