Wito umetolewa kwa viongozi wageni wa kanisa la Church of God misheni ya Bumamu kuhakikisha wanaliunganisha kanisa hilo ili kuliendeleza mbele
Wakizungumza baada ya hafla ya kuwachagua viongozi wapya 5 wa kanisa hilo kiwango cha misheni iliyofanyika katika kanisa la Mushieywe lililoko wadi ya Marama Kaskazini eneo bunge la Butere waumini na baadhi ya wahubiri wakiongozwa na Rev Johnstone Keya na Joshua Omeno wamewataka viongozi hao wapya kuhakikisha wameunganisha makanisa yote yaliyoko eneo hilo ambayo wanadai yametengana
Kwa upande wake askofu mteuliwa Rev Jackson Saya pamoja na ofisi yake wamewahakikishia waumini wa kanisa hilo kuwa wataliunganisha huku wakitoa wito kwa ofisi inayoondoka kushirikiana nao ili kuendeleza kanisa hilo
Baadhi ya viongozi walioteuliwa pamoja na Askofu huyo ni Ernest Induswe kuwa karani na Dorcas Oraka kuwa mweka hazina huku mpinzani mkuu wa askofu huyo ambaye pia alikuwa askofu wa kanisa hilo kwa miaka 11 akisusia uchaguzi huo.
By Richard Milimu