Wakaazi mjini Webuye Kaunti ya Bungoma wamemtaka gavana wa Kaunti ya Bungoma Wyclife Wangamati kutafuta njia mbadala ya kutatua mzozo unaoshudiwa baina yake na baadhi ya wakilishi wadi hasa kuhusiana na uajiri wa wasimamizi wa vijiji.

Wakizungumza na wanahabari katika eneo bunge la Webuye Magharibi wakati wa zoezi la mahojiano ya maafisa hao,wakaazi hao wakiongozwa na Edward Wekesa wamesema kuwa kuwa vijana wengi wanahangaika kwa ukosefu wa ajira hivyo basi ni bora kwa viongozi hao kutatua mzozo huo ili vijana waajiriwe.

Wakazi hao hata hivyo wamewashutumu baadhi ya watu ambao wameajiriwa  kwingine na wametuma maombi ya kupata nafasi hizo huku wakisema kuwa ingekuwa vyema kwao kuwaachia vijana wasio na ajira nafasi hizo.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE