Mashirika ya Kijamii Kaunti ya Bungoma sasa yanataka kuwepo ushirikiano mwema kati yao na serikali ya Kaunti hiyo ili kuimarisha mazingira ya utendakazi na kuboresha huduma kwa umma.

Kwenye taarifa kwa wanahabari baada ya kongamano la kila mwaka, Lumumba Wekesa ambaye ni mmoja wa wanaharakati Kaunti hiyo, amesema mashirika ya kijamii yamedharauliwa na kwamba mara kwa mara barua wanazoiandikia serikali ya Kaunti huishia kutojibiwa.

Kwa upande wake Adrian Sakwa, ameutaka utata wa uongozi unaoshuhudiwa kati ya bunge la Kaunti ya Bungoma na gavana Wycliffe Wangamati kutatuliwa ili kutolemaza utoaji huduma kwa umma.

Kongamano la mwaka huu la wanaharakati linalenga kutoa uhamasisho Zaidi kuhusu majukumu ya wanaharakati katika ushirikiano baina yao na serikali ya Kaunti jinsi anayoeleza Ezekiel Odeo ambaye ni mwenyekiti wa mashirika ya kijamii kaunti ya Bungoma.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE