Huku shule zikitarajiwa kufunguliwa kwanzia juma lijalo jumatatu tarehe 10.5.2021 kwa muhula wa tatu nchini 

Mkurugenzi mkuu wa shule ya msingi ya kibinafsi ya Hill Top Sherry Academy iliyoko kwenye barabara kuu ya Lubao kuelekea Chevoso Geoffrey Agesa ametangaza shule hiyo itapeana udhamini kwa wanafunzi walio na uwezo wa kuzoa alama 350 kwa masomo yao kwanzia darasa la tano hadi darasa la nane.

Agesa amesema kuwa wanafunzi hao bila kubagua wanakotoka hawataitajika kulipa ada zozote shuleni humo ikiwemo karo ya shule hadi watakapo maliza darasa la nane

Wakati uo huo Agesa amesema kuwa shule hiyo imeendelea kujiandaa kufunguliwa kwa shule hiyo juma lijalo kwa kujenga madarasa zaidi ili kuwawezesha wanafunzi kusalia salama kutokana na mkurupuko wa virusi vya korona

Agesa amesema karo ya shule hiyo itasalia kuwa ya chini kwa wanafunzi wengineo huku wale wa kwanzia shule ya chekechea hadi darasa la tatu watahitajika kulipa karo ya shilingi elfu tatu pekee huku wale wa darasa la nne hadi la nane watasalia kulipa karo ya shilingi elfu tatu na mia tano

Agesa amesema shule hiyo ilikalia mtihani wake wa kwanza wa kitaifa kwenye matokeo yaliyotangazwa na waziri wa elimu nchini majuma kadhaa yaliyopita huku watahiniwa 16 wakikalia mtihani huo na kuandikisha matokeo mazuri 

By Sajida Javan

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE