Wito umetolewa wa mashirika ya maziwa  kaunti ya Vihiga kutia bidii ili yaweze kufaidika na mipango mbalimbali ya ufadhili kutoka kwa serikali ya kaunti ya Vihiga ili kuimarisha uzalishaji wa maziwa katika kaunti hiyo

Haya ni kwa mujibu wa Gavana Wilbur Otichilo akizungumza katika hafla ya kuyakabidhi mashirika ya maziwa ya Sabatia jumla ya pesa milioni kumi na sita kupitia mradi wa nargp zitakazotumika na mashirika hayo kununua vifaa ili kuhakikisha uzalishaji wa maziwa katika viwanda hivyo imeimarika.

Naibu gavana wa kaunti hii daktari Patrick Saisi akizungumza katika hafla hiyo amesikitika kua japo serikali ya kaunti imejitolea kufadhili wakulima na mashirika mbalimbali kiwango cha uzalishaji wa maziwa katika eneo hili bado kiko chini ikilinganishwa na maeneo mengine.

Ni jambo ambalo limeshabikiwa na afisa mkuu katika idara ya mashirika ya jamii kaunti ya Vihiga Chris Agava.

Story by Shitemi Boaz

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE