Saa chache baada ya waziri wa elimu profesa Gorge Magoha kutangaza matokeo ya mtihani wa darasa la nane baadhi ya shule za msingi katika kaunti ya Kakamega zimesherehekea matokeo mazuri ya mtihani huo licha ya kuwepo kwa changamoto ya janga la corona mwaka uliopita.

Wakizungumza katika shule mbalimbali zikiwemo za umma na kibinafsi, walimu wakuu wa shule hizo wakiongozwa na mwalimu mkuu wa shule ya kibinafsi ya Hill school Josephat Mangala, mkurugenzi wa Fesbeth Ruth Minishi  na  mkuu wa shule ya msingi ya Kakamega Dickson Wanyangu ambao wamefurahia matokeo hayo wamesema  ni ushirikiano mwema miongoni mwa walimu na wanafunzi ambao umechangia matokeo hayo

Baadhi ya wanafunzi ambao walijizolea alama za mia nne na zaidi akiwemo Mitchele  Makungu wa Kakamega primary na Ryan Prince  wa Fesbeth wamesema ni juhudi na ushirikano wa walimu ambao ulifanikisha wao kupata alama hizo

Hata hivyo mkurugenzi wa shule ya Kibinafsi ya Fesbeth Ruth Minishi ametilia shaka jinsi matokeo ya shule za kibinafsi haya kuwa ya kuridhisha jinsi hua miaka nyingine  

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE