Hali ya huzuni imetanda katika kijiji cha Matsakha eneo bunge ka Malava kaunti ya Kakamega kufuatia kifo cha mamake marehemu daktari Hudson Alumera aliyeaga dunia mwaka jana kutokana na virusi vya corona.

Inaarifiwa Truphena Teete mwenye umri wa miaka 66 ambaye alikuwa na ugonjwa wa shinikizo la damu alifariki akitafuta matibabu katika hospitali moja kaunti ya Bungoma baada ya kukosa nafasi ya kitanda cha ICU kwenye hospitali ya rufaa ya Kakamega.

Familia hiyo ikiongizwa na mwanawe marehemu Steve Tete imesikitikia kifo cha mpendwa wao, huku wakidai ni kutokana na ukosefu wa vifaa kwenye hospitali ya rufaa ya Kakamega.

Awali waziri wa afya katika kaunti hiyo Collins Matemba alikuwa amesema kuwa kuna vitanda vya kutosha na hewa ya Oksijeni kwenye hospitali hiyo ila kifo hicho kinaibua maswali.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE