Mfanyibiashara mmoja kutoka kijiji cha Nyorotisi Kirwa eneo bunge la Likuyani kaunti ya Kakamega anayataka mashirika ya kutetea haki za wanaume kumsaidia kurejesha mkewe ambaye amenyakuliwa na mfanyikazi wake wa nyumbani.
Aggrey Masinde baba ya watoto watano anasema mkewe Irene Mwachuma Masika alimuhadaa kuwa amepokea ripoti kuwa mjombake ni mgonjwa, ambapo aliamua kuuza kuku kadhaa na kufanikiwa kupata shilingi 2500 ambazo angetumia kama nauli, pasina ya kufahamu kuwa alikuwa na njama na mfanyikazi wake kwa jina Wafula nakitani, ambaye aliponyoka naye na kima cha shilingi elfu 50 alizotoa kwenye duka lake hadi nyumbani kwao Sirisia kaunti ya Bungoma.
Mtetezi wa haki za kibinadamu eneo hilo Eliminah Mmbone anasema wamechukua hatua ya kusafiri hadi nyumbani kwao mhusika ili waweze kumrejesha Irene, akitaka mfanyikazi huyo kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Story by Samson Nyongesa