Aliyekuwa Seneta wa kaunti ya Kakamega Bonny Khalwale sasa anataka usimamizi wa kiwanda cha sukari cha Butali na kile cha West Kenya kushughulikia tatizo la wakulima wa miwa na wala sio  kuwatumia madalili kuhujumu sekta hiyo muhimu

Akizungumza katika eneo bunge la Malava Khalwale amesikitika kuona wakulima wengi wakipitia hali ngumu kukidhi mahitaji yao ikiwemo kushindwa kugharamia malipo ya watoto wao shuleni kufuatia madai ya kunyimwa vibali vya kuvuna zao la miwa

“I want to tell the management of Butali Sugar Company, you were not given the opportunity to harass the farmers you were given the opportunity to serve them equally. Wacha wakulima wakuje kuchukua permit wenyewe.” Alisema seneta Bonny Khalwale

Kauli ya khalwale inajiri siku chache tu baada ya wengi ya wakulima wakilalamikia madai ya kunyimwa vibali vya kukata miwa yao mbali na kuitishwa rushwa na maafisa wa kampuni hizo mbili ili kukabidhiwa vibali hivyo maarufu kama permit.

“Mpaka tuhongane pesa na kama una pesa unaambiwa ulipe mahindi gunia moja kwanini tunafanyiwa ivyo. Sasa watoto wako nyumbani tujui tutafanya nini, tunashangaa lazima tuhongane ndo tukatiwe miwa ama sukari inatoka inche ya nnchi?”Malalamishi ya Wakaazi

Kwalwale sasa anawataka wawakilishi wadi katika bunge la kaunti ya kakamega kubuni sheria mwafaka itakayosaidia kudhibiti sekta ya miwa kwa manufaa ya mkulima wa ngazi ya chini

Story by imelda lihavi

sadmin

By sadmin

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE