Watu kadhaa nchini bado wanahifadhi fedha zao kinyumbani wakitumia vyombo maalum vilivyoundwa kuhifadhi pesa zao
Kwenye kaunti ya Kakamega wanakijiji hutumia mbinu hii kama uwekaji wa fedha zao ambazo huenda wakazitumia kwa shughuli maalum walizoziandaa za usoni hasa ikiwemo biashara
Baadhi ya waliozungumzia mbinu hii ya kuhifadhi fedha wanaamii kuwa mbinu hiyo ni bora hasa kulingana na mapato yao ya kinyumbani.
Licha ya baadhi kutumia mbinu hii bado kuna wale wanashikilia na kuamini mbinu zilizoko za kisasa za kuhifadhi hela zao.wanashikilia kwamba fedha si vyema kuhifadhiwa nyumbani kwani chochote kinaweza tokea na kuhathiri kiwango hizo cha fedha zilizohifadhiwa.
By Austin Shambetsa