Baadhi ya viongozi wa kidini katika kaunti ya Kakamega sasa wanaitaka serikali kuweka uzito kwa maswala ya wazee ambao wamefikisha umri wa miaka sabini na zaidi na kuona kwamba wanasaidika

 Wakiongea kwenye hafla ya kuadhimisha miaka sabini ya mchungaji Charles Omuroka mjini Kakamega, viongozi hao kupitia kwa mchungaji Wilfred Mumia wamesema inasikitisha kuwa wakongwe wengi hawana mapato ya kujikimu ikizingatiwa hali ngumu ya maisha

Omumia vile vile amewataka viongozi serikali kuzingatia mawaidha ya wazee ambao wangali na uwezo wa kutoa huduma kwa serikali

Apostle Charles Omuroka ambaye alisherekea kuadhimisha miaka sabini ameunga mkono usemi huo na kusema huwa vigumu hata kwa wazee kupata huduma katka baadhi ya ofisi za serikali

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE