Mtoto mvulana wa miaka 16 alifikishwa katika mahakama ya Kakamega na kushtakiwa na kosa la kuuwa mwalimu wa shule ya msingi akitumia jiwe.
Brighton Mucheru alifikishwa katika mahakama ya Kakamega mbele ya hakimu mkuu wa mahakama hiyo Dolphin Alego na kushtakiwa kuwa mnamo tarehe 13/3/2021 katika kijiji cha Shihumbu kata ya Khayega eneo bunge la Shinyalu kaunti ya Kakamega alimuuwa Maurice Khataka kwa kumpiga na jiwe.
Hata hivyo mshukiwa alikanusha mashtaka dhidi yake huku mahakama ikiamuru apelekwe kwenye rimande za watoto za Kakamega huku uchunguzi zaidi kupitia kwa afisa ya DCI kaunti ndogo ya Kakamega Mashariki ukiendelea.
Kesi hiyo itatajwa yarehe 8/4/2021 na kusikizwa mnamo tarehe 17/6/2021.