Hali ya huzuni imetanda katika maeneo ya Harambee  wadi ya Kholera eneo bunge la Matungu kaunti ya Kakamega baada ya mtoto msichana ambaye ni wa darasa la sita kufariki papo hapo baada ya kugongwa na gari ndogo kwenye barabara kuu ya Mumias kuelekea Bungoma jumatatu jioni.

Kulingana na walioshuhudia ajali hiyo wanasema kuwa marehemu alikumbana na mauti hayo alipotumwa na wazazi wake kuenda dukani ndipo gari hilo lililokuwa likiendeshwa kwa mwendo wa kasi likiyumbayumba barabarani kumgonga na kufariki papo hapo.

Hata hivyo walioshuhudia wanasema kuwa baada ya ajali hiyo dereva wa gari hilo alitoweka huku mwili wa mwendazake Ukiihifadhiwa kwenye chumba cha maiti katika hospitali ya misheni ya Mtakatifu Maria Mumias .

By Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE