Timu ya wachezaji wa zamani iliisakama timu ya walimu kutoka eneo bunge la Malava mabao matatu dhidi mawili kwenye mechi ya kirafiki iliyoandaliwa katika uwanja wa shule ya upili ya wavulana ya Lugusi.
Itimu hiyo ya wachezaji wa zamani iliongozwa na aliyekuwa mchezaji wa Harambee Star Antony Okumu ambaye pia ni katibu mkuu wa FKF kaunti ya Kakamega na meneja wa timu ya Kakamega Homeboyz Bonface Imbenzi huku mwakilishi wa vijana katika shirikisho la kandanda FKF kaunti ya Kakamega Enoch Lucheveleli akiongoza kikosi cha walimu.
Akizungumza baada ya mechi hiyo yenye msisimko nahodha wa timu hiyo ya walimu wa Malava Enoch Lucheveleli aliridhishwa na mechi hiyo pamoja na matokeo .
By Richard Milimu