Wafanyibiashara katika soko la Malaha eneo bunge la Mumias Mashariki kaunti ya Kakamega waliwachagua viongozi wao watakaowawakilisha huku Johnstone Agostine Mukeka akichaguliwa kama mwenyekiti wao kwenye uchaguzi uliosimamiwa na maafisa wa serikali ya kaunti ya Kakamega.

Wengine waliochaguliwa ni  John Okalo kama naibu mwenyekiti, Caroline Nanzala mweka hazina ,Lucy Namisi mwakilishi wa kina mama na Fred Mangwana kama afisa wa kushughulikia maslahi ya wanachama wa soko hilo .

Uchaguzi huo ulisimamiwa na mtawala anayesimamia wadi ya Isongo/ Makunga/ Malaha katika serikali ya kaunti ya Kakamega bi, Clare Wambulwa huku akisema kuwa viongozi hao watafanya kazi pamoja na serikali ya kaunti na ile ya taifa kuwakilisha wafanyibiashara wa soko hilo.

Kwa upande wake Johnstone Mukeka baada ya kutangazwa mshindi aliwashukuru kuchaguliwa kwake huku akiwataka walioshindwa kwenye uchaguzi huo kushirikiana na afisi ilichaguliwa kuwashughilikia wafanyibiashara .

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE