Familia moja kutoka kijiji cha Mufungu, kata ya Chesikaki eneobunge la Mlima Elgon imetoa wito kwa viongozi na wahisani mbalimbali kujitokeza na kuwapa msaada wa dawa baada ya watato tano kuathirika na wadudu aina ya funza.

Kulingana na bi Margaret Simuli Watima, nyanyake watoto hao anasema imekuwa vigumu kwake kudhibiti funza hao ambao wamekuwa kero kwa wajuku wake akidokeza kuwa mara nyingi funza hao huwavamia watoto hao msimu wa kiangazi.

Aidha bi Simuli anasema kufwatia hali yake ya uchochole imekuwa vigumu kwake kupata dawa ya kuwatibu wajukuu wake, na kutoa wito kwa wahisani kuwapa usaidizi wa dharura.

Baadhi ya majirani wakiongozwa na Ben Obama wakitoa wito kwa uongozi wa kaunti ya Bungoma na wadi ya Chesikaki kuingilia kati upesi na kushughulikia swala hilo ambalo limekuwa kero kwa nyingi za familia eneo hilo.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE