Kufwatia kutiwa mbaroni kwa mwanabodaboda mmoja eneo la Makunga kaunti ndogo ya Mumias Mashariki sasa wanabodaboda sokoni humo wamejitokeza na kukashifu vikali kitendo hicho
Wakiongozwa na Caleb Okumu wahudumu hao wa bodaboda wametaka hatua kali ichukuliwe dhidi ya mhusika
Wanabodaboda hao aidha wamewatahadharisha wenzao dhidi ya vitendo sawia
Vijana hao vilevile wamekanusha kuwa sekta hiyo ya bodaboda hutumika kutekeleza uhalifu wakisema kuwa ni visa Kama hivyo tu vinavyotumika kuwaharibia saifa
Mshukiwa anazuiliwa katika kituo cha polisi Cha Isongo wilayani Mumias Mashariki akingoja kufikishwa mahakamani
By James Nadwa