Migomo ya mara kwa mara miongoni mwa wafanyikazi wa sekta mbali mbali humu nchini ndio sababisho la migomo inayoshuhudiwa miongoni mwa wanafunzi,
Ni usemi wa padre wa parokia ya kanduyi kaunti ya Bungoma Dominic Osianji
Akizungumza kwenye hafla ya mazishi ya mwendazake nduguye mbunge wa Kanduyi Kizito Wafula huko Ranje kwenye eneo wakilishi wadi ya Bukembe mashariki eneo bunge la Kanduyi, Padri Osianji amesikitikia matukio ya hivi punde ya ukosefu wa nidhamu miongoni mwa wanafunzi huku akikariri kuwa wizara ya elimu inahitaji kuweka mbinu mbadala ya kukabiliana na visa hivyo bila kuekea wazazi gharama ghali inayotokana na visa hivyo
Wakati uo huo padre huyo ametoa changamoto kwa wazazi kuwa waangalifu kwa wanao haswa likizo nyingine ya wanafunzi inapokaribia huku akitaja visa vya uaviaji mimba miongoni mwa wanafunzi wa kike kama moja wapo ya mbinu zinazotumika na jamii kwa ujumla ili kuendeleza uovu.
Usemi wa padre Osianji unakuja siku chache baada ya kuibuka mjadala mkali wa kurudisha adhabu ya kiboko shuleni,usemi unao onekana kukinzana na pendekezo hilo
Ikumbukwe kuwa tangia kufunguliwa kwa shule baada ya kipindi kirefu cha likizo isiyo ya kawaida iliyosababishwa na mkurupuko wa virusi hatari vya covid_19 mapema mwaka jana,shule nyingi kote nchini zimeshuhudia visa vya utovu wa nidhamu huku kaunti ya Bungoma ikiorodheshwa miongoni mwa kaunti zilizoadhirika pakubwa kutokana na visa hivyo.
Story by Hillary Karugani