mimba za mapema ni swala sugu linalowaathiri wakenya sasa. kulingana na mchungaji wa kanisa la pesa pst david andayi anasikitikia kuwepo kwa mimba za mapema miongoni mwa watoto walio chimi ya umri wa miaka kumi na nane.

mimba za mapema ni kama kizungumkuti nchini na sasa watoto wetu leo wanapatikana na mimba hata wakiwa shuleni

akizungumza na idhaa hii mchungaji andayi anawasihi wazazi kuchukua jukumu lao la kuwalea wanao bila kulegeza kamba na kuwaelekeza ipasavyo wakati ampapo wako nyumbani na pia shuleni.

akizungumza na idhaa hii pst david andayi wa Kanisa la pefa, anawasii wazazi wachukue jukumu lao kwa maaana kwa sasa wazazi wamelegeza kamba kwa kujukumika kwa kuwalea watoto na kuwaelekeza ipasavyo

anawahiza wanafunzi kuwa si vyema kufanya ndoa za majaribio kwa maana zinasababisha mimba za mapema na kungojea hadi wakati watakapofikisha umri huo wa kuoa na kuolewa ili kujiepusha na dhambi zinazotokana na mimba za mapema. na kwa walimu wana jukumu la kuwaangalia wakati wapo shuleni na kuwafunza kuwa watiifu.

watoto wakiwa shuleni ni jukumu la Mwalimu kumwangalia na wakati watoto wako nyumbani ni jukumu la mzazi na hivyo anawaelekeza wazazi kutia bidii kwa kuwalea watoto wao

anawasihi wanafunzi kutulia wakati wako nyumbani na wakati wanapo maliza mitihani yao mpaka watakapo fikisha huo umri wa kuoa na kuolewa ili kuepusha dhambi zinazotokana na mimba za mapema

By Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE