Accident Ahead sign illustration

Mhudumu mmoja wa bodaboda amefariki papo hapo huku abiria wake wawili wakisazwa na majeraha mabaya kwenye barabara ya Kakamega-Webuye karibu na kituo cha mafuta cha Holiday mjini Malava.

Kulingana na waliyoshuhudia ajali hiyo,ni kuwa mwendazake alikuwa akiendesha pikipiki kwa mwendo wa kasi ambapo aligonga kwa nyuma trekta ya kubeba miwa ya kampuni ya butali na kupelekea kifo chake. Hata hivyo mwenyekiti wa wahudumu wa bodaboda Francis Mulievi amewataka wahudumu hao kuendesha pikipiki zao kwa uwangalifu ili kuepuka maafa yanayotokana na ajali za barabara.

Tayari mwili wa marehemu umechukuliwa na maafisa wa polisi na kupelekwa kwenye chumba cha wafu cha hospitali ya kaunti ya Kakamega huku majeruhi wakilazwa hospitalini mjini Malava kwa matibabu zaidi.

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE