Aliyekuwa mwanafunzi bora kwenye mtihani wa KCPE mwaka huu katika shule ya msingi ya Muyai mjini Bungoma anaomba usaidizi wa kifedha kugharamia matibabu ya mguu wake wa kushoto ulio na uvimbe ambao umedumu kwa miaka tisa.
Kevin Barasa aliyepata alama 401 kwenye mtihani wa KCPE anahofia kuwa huenda akatatizika zaidi katika shule ya upili endapo mguu huo hautatibiwa kwa wakati.
Kwa mujibu wa Esther Kasyoki mamake Kevin, uvimbe huo ulianza mwaka 2012 akiwa darasa la pill, na kwamba familia hiyo haina uwezo kupata shilingi Elfu Mia Tatu Hamsini zinazohitajika kumfanyia upasuaji.
Wakati mwingi, mwanafunzi huyo alikosa kuhudhuria vipindi vya masomo kufuatia maumivu kwenye mguu wake jinsi anavyoeleza Mwalimu Mkuu wa shule ya Muyai Godfrey Ngoya.