Wahumini wa kanisa la Faith Believers tawi la Murumba ilioko wadi ya Butsotso Mashariki eneobunge la Lurambi kaunti Kakamega wakiongozwa na pastor Oliver Kenzi  wameonyesha furaha isiyo na kipimo kwa kutembelewa na wageni mbalimbali wakiwemo makasisi kutoka nji ya america. 

 Washirika wakanisa hili pamoja na wale wamakanisa mengine walifurika ndani ya kanisa ili kupata injili kutoka kwa wageni ambao pia ni watumishi wa Mungu.kando na kutangaza injili waliwapa waumini vyakula mbalimbali,malazi pamoja na biblia kwa wale ambao hawana uwezo wa kununua.     

  Hata hivyo aliyewaongoza akiwa ni mhubiri kutoka Nnji ya America kwa jina Philip’s alisema kuwa lengo lao kuu ni kueneza njili hapa Kenya na pia kuwapa waumini chakula cha shibe kuongezea kwa kile cha kiroho.

  Mchungaji wa kanisa hilo kwa jina Oliver Kenzi alichukua fursa ya kurudishia wageni shukrani wakiwemo wachungaji wa makanisa mengine hapa Kenya na kusema kwamba aliwapa wageni hao fursa ya kuhubiri injili ili wakristo wote wakaze mwendo katika ukristo

Vilevile viongozi wengine wa kanisa hili la Faith Believers pia walikuwa na furaha na kurudisha shukrani zao kwa bw Philip kutoka Amerika pamoja na wote walioandamana nao. 

Kiongozi wa vijana Veronicah naye hakuwachwa nyuma kwani alionyesha tabasamu usoni na kuhimiza vijana waige mfano wa wale waliowatembelea  na wamrudie Mungu na kujikaza kwa kazi ya Kanisa

By Linda Adhiambo

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE