Zaidi ya watu 100 wafamilia tatu kutoka kijiji cha Nanyeni eneo bunge la Matungu kaunti ya Kakamega wamelazimika kugesha nje kwa kijibaridi baada ya nyumba zao za kifahali kubomolewa baada ya mahakama kutoa Kibali cha familia hiyo kuondolewa.
Vincent Nambiro anasema dadake Ann Wesonga Nambiro ambaye ni mbunge mteule katika bunge la Kakamega nduguye Michael Almasi Ongalo na babake marehemu Peter Nambiro waliwasilisha kesi mahakamani, wakidai familia hizo chini Ibrahim Wakhanyanga, Abdalla Wawere na Hussen Munyendo wanaishi kwenye kwenye shamba hilo la hekari 17 kinyume cha sheria.
Hata hivyo watatu hao wanasema baba ya walalamishi mwendazake Peter Nambiro alitumia njia ya mkato kunyagua shamba lao ambalo ni 1065 kinyume na ile namba wanayosema ya 1225 na yao 1226 wakitaka serikali kuwasaidia.
Aidha mbunge wa eneo hilo amekashfu hatua ya polisi kutumiwa visivyo kuwafurusha wahusika kwenye shamba hilo, huku akitoa msaada wa malazi na vyakula kwa walioathirika, ambao kwa sasa wamekimbilia kuishi kwenye Msikiti.
By Linda Adhiambo