Naibu gavana wa jimbo la Kakamega prof.Philip Kutima amesisitiza umuhimu wa wakazi wa kaunti hiyo kuenedela kuafuata kanuni za wizara ya afya ili kuzuia mambukizi zaidi ya virusi vya corona miongoni mwao

Akizungumza kwenye hafla ya mazishi ya mama Emily Iyaka  Angatia mkewe aliyekuwa kwa wakati mmoja mbunge wa Malava marehemu Joshua Angatia katika kijiji cha Shamoni eneo bunge la Malava, Kutima amesikitikia kuongezeka kwa vifo vingi vinavyotokana na homa ya corona huku akiwarai wakazi wa kaunti ya Kakamega kuzingatia kikamilifu masharti ya serikali kupitia kwa wizara ya afya katika kuzuia msambao zaidi wa virusi hivyo hatari.

Naye mbunge wa Malava Malulu Injendi ambaye pia alihudhuria mazishi hayo amehoji kuwa wakati umefika sasa kwa viongozi kutoka eneo la Magharibi kushirikiana na kumuunga mkono kinara wa chama cha ANC Musalia Mudavadi kuwania kiti cha urais kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Aidha malulu ametumia fursa hiyo kuilimbikizia lawama serikali ya kitaifa kufuatia kuboromoka kwa viwanda muhimu katika eneo la magharibi tofauti na maneo mengine nchini.

Kauli ya injendi imepigwa jeki na mwakilishi wa wadi ya kabras magharibi davidi ndakwa ambaye amewataka wakenya kufuata maagizo ya wizara ya afya ili wawe salama.

By Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE