Wanaharakati wa mazingira pamoja na muungano wa wafanyibiashara wa hoteli katika kaunti ya Transnzoia wamejitokeza na kukemea mradi unaopangwa kujengwa katika msitu ulioko mlima elgon.
Wakiongea na wanahabari mjini kitale wanaharakati hao wakiongozwa na immaculate kipyesang wanasema ujenzi wa mradi huo wa serekali kuu wa kujenga kituo kimoja cha mpaka Kati ya kenya na uganda katika eneo hilo litachangia pakubwa uaribifu wa mazingira.
Eneo hilo ambalo liko katika eneo bunge la endembess kaunti hii ya Transnzoia linapangiwa kutumia na nchi hizi mbili za kenya na uganda kwa shughuli za ukaguzi wa magari, mizigo,na stakabadhi za wasafiri wanaotoka na kuingia kati ya nchi hizi mbili.
Aidha wanaharakati hao wanasema iwapo ujenzi kituo hicho utaendelea utaadhiri chemi chemi za maji katika eneo hilo ikikumbukwa kuwa msitu huo una vyanzo vingi vya mito zinazotiririka kutoka eneo hilo
Wametishia kuelekea mahakamani kusitisha ujenzi wa mradi huo huku wakiomba serekali kuu kuingilia Kati na kuokoa uaribifu wa msitu huo
By Richard Milimu