Ni afueni kwa wanafunzi na wakazi wa  kijiji cha Irenji wadi ya Isukha Magharibi eneo bunge la Shinyalu baada ya daraja la Shianda ambalo wamekuwa wakivuka wakitumia miti ili kufika  shuleni kujengwa.

Ni daraja lililotishia maisha ya wengi wa wakazi, haswa wanafunzi ambao hulazimika kuvuka kila siku  kuelekea shuleni, tatizo hili likikabiliwa na mkazi mmoja kutoka eneo bunge hili la Shinyalu, daktari Anthony Lungaho, mkurugenzi mkuu wa Nuclear Energy kama njia moja ya kuisaidia jamii eneo hili, na wakazi hawangeficha furaha yao.

Dakta Lungaho amesikitishwa na baadhi ya viongozi waliochaguliwa kaunti ya Kakamega wanayoyafumbia macho masaibu ya wakazi na kuwarai kuwajibikia majukumu yao na kuhakikisha kuwa miradi ya maendeleo inawafikia wakazi mashinani bila ya ubaguzi.

Akizungumza katika kijiji hiki cha Irenji alipofika kukagua daraja lililomgharimu zaidi ya shilingi alfu mia moja kulijenga, Lungaho anafichua kuwa ataendelea kuwanufaisha wakazi mashinani

By Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE