Muda mfupi baada ya rais Uhuru Kenyatta kutoa marufuku ya kutoka na kuingia katika  kaunti  tano zilizokuwa kwenye marufuku hayo ili kuzuia virusi vya korona, mtafiti mkuu ukanda wa Afrika kutoka shirika lisilokua la serikali  duniani linaloshughulikia ulinzi wa raia pamoja na kudhibiti hali ya dharura (ICPEM)  Adrian Meja, amehoji kuwa nchi nyingi zilizoweza kuzuia kusambaa kwa korona zilifaulu kufwatia kutia marufuku ya kutoka na kuingia  na hio ndio njia rahisi na dhabiti ya kuweza kuzuia usambaaji wa covid 19.

Meja, ambaye pia ni mwaniaji wa kiti cha ubunge eneo la Shinyalu aliongeza kuwa, njia rahisi ya kupunguza kusambaa ugonjwa huo ni kukaa nyumbani bila kutangamana na watu na kama ni lazima utoke nyumbani basi sharti uvalie barakoa, uoshe mikono kwa maji na sabuni kisha utumie sanitaiza

By Tomcliff Makanga

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE