Wito umetolewa kwa kundi la wanafunzi ambao hawangeweza kujiunga na vyuo vikuu wapate kujiunga na vyuo vya anuai pamoja na vya ufundi ili kuweza kujiimarisha kielimu kama vile kusomea uandishi wa habari ili kukuza vituo vya habari na runinga katika kaunti ya Kakamega.

Ni usemi wake mwakilishi wadi ya Shirere mwalimu David Ikunza alipokuwa katika sherehe ya kuadhimisha miaka mitano ya runinga ya pendo tangu kuenda hewani.

Ni usemi uliopata uungwaji mkono naye mwakilishi wadi ya Butsotso ya Mashariki Mathew Nyongesa  pamoja na mwaniaji kiti cha ubunge eneo la Shinyalu mheshimiwa Adrian Meja ambao walikuwa wamehudhuria hafla hiyo.

Meja kwa upande wake aliwapongeza wana pendo kwa kuadhimisha miaka mitano na kuwaomba wazidi kukuza talanta na kuboresha upeperushaji wa habari katika kaunti ya Kakamega.

By Tomcliff Makanga

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE