Imekua shangwe na nderemo mjini Kakamega kwa washikadau, wamiliki pamoja na wanahabari wa kituo cha televisheni cha Pendo walipokua wakiadhimisha miaka mitano tangu kuenda hewani.
Ni furaha iliyodhihirishwa naye mkurugenzi mwanzilishi ambaye pia ni mmiliki wa kituo hicho mama askofu Sofia Malenya ambaye aliwashukuru watazamaji pamoja na halmashauri kuweza kujumuika nao.
Vincent Mumia mwanahabari wa kituo hicho pia aliweza kuonyesha furaha yake na pia kuhimiza vituo vya habari katika kanda ya Magharibi vizidi kukuza talanta ya vijana chipuka
Aidha, katibu mkuu wa muungano wa wanahabari kanda ya Magharibi Nathan Ochunge aliweza kuwapongeza na kuwasihi wazidi kutia bidii katika upeperushaji wa habari katika kanda ya Magharibi kupitia kituo hicho
Hata hivyo, Ochunge amewaonya wamiliki wa vituo pamoja na wanahabari bandia ambao hawajaidhinishwa na Tume ya Mawasiliano ya Kenya dhidhi ya kuenda hewani. Amewaomba kila mwanahabari kuongeza ustadhi kazini na pia kuhakikisha ameidhinishwa na tume ya mawasiliano bila kusahau, wapate kujiunga na muungano wa wanahabari ili waweze kutatua shida zao kwa pamoja
By Tomcliff Makanga