Chaguzi wa wakurugenzi wapya wa viwanda vya majani chai katika kaunti ya Kisii ulifanywa kwa njia ya amani hii leo licha ya ukinzani mkali wa awali kutoka baadhi ya wakulima na wakurugenzi wa zamani.
Katika uchaguzi uliofanyika katika shule ya Tendere, mji wa Ogembo, wakurugenzi kadha walitemwa na wapya kuteuliwa kwa kile kionekana ufanisi wa kwanza wa serikali kutia msasa usimamizi wa sekta ya majani chai nchini.
Wakurugenzi walioteuliwa hata hivyo waliahidi kupigania haki ya mkulima kwa njia ya haki ili kuona kwamba wamepata tija kutoka juhudi zake.
By Richard Milimu