Ikiwa ni siku ya tano kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza kuripoti shuleni, hali bado ni ngumu kwa Vivian Amali aliepata alama 309 katika shule ya msingi ya Angorum baada ya mzazi wake kushindwa kumlipia karo katika shule ya upili ya wasichana ya St Monica alikoitwa.

Katika eneo la Aget wadi ya Angorum eneo bunge la Teso kusini nampata Vivian Amadi nje ya maduka akiwa na huzuni mpango wake wa kujiunga na shule ya upili ya wasichana ya matakatifu Monica Chakol ikisalia kitendawili.

Akidondokwa na machozi Celestine Wanyama ambaye ni mamake Vivian na ambaye anaishi kwa nyumba ya kukodi ameambia idhaa hii kwamba huenda Amadi akakosa kutimiza ndoto yake kutokana na hali ngumu ya kimaisha anayopitia na wanawe wanne mumewe akimtelekeza kwa miaka kadhaa.

Kilio chake kimeungwa mkono na Mwanaharakati Eunice Adhiambo ambaye ametoa wito kwa wahisani kujitokeza kuwezesha binti huyu kutimiza ndoto yake.  

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE