Zaidi  ya watu 800 waliokuwa wafanyikazi wa kiwanda cha kusaga miwa cha Mumias wameitaka serikali kuingilia kati na kuwasaidia kupata marupurupu yao ya zaidi ya shilingi bilioni mbili wanazodai kampuni hiyo Jambo wanalosema limepelekea kuishi katika hali ya uchochole wengine wao wakijitoa uhai.

Wakiongozwa na Vitalisi Makokha, Patrick Mutimba na Johnson Barasa wanasema miaka nenda rudi wamekuwa wakiomba serikali kuwasaidia bila mafanikio huku wakiendelea kusakamwa na hali ngumu ya maisha wakimtaka rais Uhuru Kenyatta atakapokuja eneo la Magharibi kuwakumba waliokuwa wafanyikazi wa kampuni hiyo.

Huku wafanyibiashara na wakulima eneo la Mumias chini ya Alex Ombayo Mutuli wakisema hali hiyo imepelekea ongezeko la visa vya uhalifu sawa na ubakaji eneo zima la Mumias wakitaka rais Uhuru Kenyatta kufufua kiwanda hicho.

By Lindah Adhiambo

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE