Mwanafunzi mmoja wa kidato cha tatu katika shule ya upili ya wavulana ya Burangasi katika eneo bunge la Navakholo kaunti ya Kakamenga anazuiliwa katika kituo cha polisi eneo hilo kwa madai ya kuteketeza bweni la shule hiyo.

Kulingana na kamanda wa polisi eneo hilo la Navakholo, Richard Omanga, mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 19, baada ya kuhojiwa, amedai alichochewa kufanya kitendo hicho “kutokana na mazingira mabaya shuleni humo”.

Aidha, Omanga amesema mwanafunzi huyo, alikiri kutumia bangi, madai ambayo kamanda huyo wa polisi anasema polisi bado wanachunguza.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Steven Wafula, hata hivyo, amesema wanafunzi wote 40 ambao hulala ndani ya bweni hilo wako salama.

“Bweni lenyewe halijachomeka. Ila ni magodoro mawili na malazi ya wanafunzi wawili ambao hulala kwa vitanda hivyo,” Wafula alisema akiongeza kuwa wamewahamisha wanafunzi hao 40 kwenye bweni jingine kwa sababu “wanaweza kuwa na uwoga”.

Omanga sasa anawataka walimu wa shule kuhakikisha wanafunzi wanakaguliwa vilivyo wanapoingia shuleni.

“Inatakiwa wakaguliwe na waweze kuchunguzwa pamoja na vitu vyao wanavyoingia navyo shuleni ili wasije wakaingiza vitu hatari shuleni,”

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE