Wito umetolewa kwa wazazi kutoka kaunti ndogo ya Cheptais eneobunge la Mlima Elgon kuhakikisha wanawarejesha wanao shuleni ili kuendelea na masomo yao kama njia moja itakayowawezesha kujikimu siku za usoni.
Akihutubu baada ya kuzuru vyama vya ushirika mbalimbali katika wadi ya Chesikaki naibu kamishna wa kaunti ndogo ya Cheptais Samwel Towet, anasema ni lazima wanafunzi wote warejelee masomo yao huku akiwasihi kushirikiana kwa karibu na vyombo vya usalama ili kukabili uwezekano wa utovu wa usalama.
Aidha Towet amewashauri wakaazi kutilia maanani kilimo cha kahawa akisema kitawawezesha kujikimu kimaisha.
Amepongeza baadhi ya vyama vya ushirika eneo hilo kwa kuanzisha miradi mbalimbali ambayo anasema itawafaidi pakubwa wakulima.
Story by Richard Milimu