Hali ya majonzi imetanda katika kijiji cha Shikoti wadi ya Butsotso mashariki eneo bunge la Lurambi kaunti ya Kakamega baada ya mwanaume wa miaka 37 Kwa jina Simon Akhonya kujitia kitanzi Kwa madai ya kumpata mkewe akiongea na mwanaume mwingine nje ya nyumba yake nyakati za usiku.

Wakizungumza na wanahabari Mamake marehemu Christine Awinja pamoja na Wana familia wanasema kuwa mwendazake kabla ya kujiua alidai kuwa alipokuwa akirejea nyumbani alimfumania mkewe Elizabeth Kutekha akishiriki ngono na mpango huyo wa kando nyuma ya nyumba yake jambo lililopelekea kujitia kitanzi.

Aidha familia hiyo ya mwendazake inadai kwamba mwasiriwa na mkewe wamekuwa na ugomvi wa mara Kwa mara.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha maiti katika hospitali ya rufaa mjini Kakamega ukingojea kufanyiwa upasuaji kubaini chanzo cha kifo hicho.

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE