LUBAO FREQUENCY MODULATION LIMITED

Uniting Communities
  1. Listen to Lubao FM Live 102.2 FM

Live now:

Up next:

Viongozi wa kanisa kukashifu ufisadi nchini Kenya

Muungano wa dini kaunti ya kakamega wasema jaji mkuu Maraga  ameiacha nchi ya Kenya katika changamoto ya ufisadi.

 Muungano huo kupitia mwenyekiti wake askofu Nicholas Olumasai umedai kiwango cha juu cha ufisadi katika taifa la kenya kumepelekea nchi kuzama katika msukosuko wa kiuchumi.

 Akizungumza kwenye hafla moja ya matanga katika kijiji cha Isembe kata ndogo ya Shibuli kakamega ya kati mwenyekiti huyo pamoja na shirikishi wa muungano wa Tuinuane kaunti ya kakamega Evans Shimonyo wamekashifu vikali wanasiasa nchini kwa kukosa kutii masharti ya afya juu ya homa ya corona .

Wakati uo huo swala la BBI bado lingali linatingiza vichwa vya wakenya huku viongozi wakitaka serikali kushughulikia hali mbaya ya uchumi na maslahi ya wahudumu wa afya jinsi mshirikishi huyo na aliyekuwa diwani wa Butsotso  ya kati Benedict Ambundo wanasema .

Story by James Boaz Shitemi

Charles Oduor

Read Previous

MWANAUME AFARIKI KWA KUJITIA KITANZI KAKAMEGA KWA KUDAI KUMPATA MKEWE AKILA URODA NA MPANGO WA KANDO

Read Next

VIJANA WAZOZANA KAUNTI YA BUSIA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *