Kundi moja la vijana katika kaunti ya Busia chini ya vuguvugu la THE ALLIANCE BUSIA YOUTH ASSOCIATION limelisuta baraza la kitaifa la vijana la National Youth Alliance afisi ya Busia chini ya kiongozi wao Benjamin Sireka kwa madai ya kushindwa kupigania ajenda za vijana badala yake wameanza kujihusisha na siasa zisizo na manufaa kwa uchumi wa vijana.

Wakiongozwa na Eng’orit Musa na Maurine Ramoya, wanasema baraza la vijana kaunti ya Busia limeshindwa kupigania maslahi ya vijana badala yake linatumiwa na baadhi ya wanasiasa ili kuzuia vijana kunufaika na mgao wa ugatuzi mbali na kupora fedha za baraza hilo kwa manafuaa ya kibinafsi.

Aidha wamemtaka mwenyekiti wa baraza la vijana kaunti ya Busia Benjamin Sireka kuweka wazi matumizi ya fedha ambazo wamepokea kutoka kwa serikali ya kitaifa tangu waingie afisini miaka minane iliyopita mbali na kung’atuka uongozini.

Story by Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE