Huenda jamaa ya mzee aliyeaga katika eneo bunge la Ikolomani miezi kumi na nane iliyopita na kuzuiliwa kuzikwa kwa kipande alichonunua yapata miaka 45 iliyopita kwa kutokamilisha malipo wakaendelea kumuombolelezea kwenye chumba cha wafu Mukumu baada ya wenye shamba kuendelea kupinga kuzikwa kwake.

Akizungumza nyumbani kwake  kiongozi wa familia inayosemekana kupinga wakidai kulipwa deni lao kwanza Charles Kangayia amesema kuwa hawawezi kukubali marehemu kuzikwa kwenye shamba hilo kabla ya kulipa deni.

Ni kauli ambayo imeungwa mkono na dadake Charles  Consolata Kangayia na kusema kuwa marehemu amekuwa akimcheza babayao hadi kufariki kwake na sasa hawatakubali mchezo huo kuendelea.

Siku ya jumatatu familia ya marehemu ambaye angali katika chumba cha wafu kwa muda wa miezi 18 ikiongozwa na Alfred Musavi , ilidai kuwa  marehemu baba yao alinunua shamba hilo hekari 2 kwa  mzee ambaye pia ni marehemu James Kangayia mwaka 1975 kwa shilingi 6000 ambaye aliaga bila jamii hizi mbili kulumbana mwaka 2009, na sasa mzozo ulianza mwaka 2019 alipoaga baba yao jamii ya aliyewauzia shamba ikidai kuwa wana deni na hawawezi kumzika mzee huyo ndani ya shamba hilo. By Kennedy Babangida

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE